MECHI ya kirafiki ya kimataifa ambayo imekuwa ikidaiwa kuwa itafanyika hivi karibuni kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe ipo kwenye hatihati ya kufanyika.
Mchezo huo ambao ulipangwa kufanyika Aprili 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya shabiki wa Simba, Azim Dewji, unaweza kukwama kutokana na ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Chanzo muhimu kutoka ndani ya benchi la ufundi la Simba kuwa uwezekano wa kuwepo kwa mechi hiyo ni mdogo, kwani akili yao yote ipo kwenye ligi kuu na michuano hiyo ya kimataifa.
“Kiukweli ukiangalia ratiba ya ligi imetubana sana, mechi mbili zinafuatana kabla ya kucheza na wapinzani wetu Al Ahli, ni vigumu kucheza mechi ya kirafiki na Mazembe.
“Hiyo taarifa yenyewe ya mechi uongozi haijatufikia rasmi, taarifa tunasikia kwenye vyombo vya habari pekee, tumependekeza tufanye mazoezi na kucheza mechi za ligi za kujiandaa kabla ya kucheza na Al Ahli,” kilisema chanzo hicho.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Rage, alipoulizwa kuhusiana na hilo, alisema: “Suala hilo anatakiwa kuulizwa muandaaji wa mechi hiyo (Dewji), sisi hatuwezi kujibu lolote, wao Mazembe kama wakija tutacheza nao.”
SIMBA YAKATAA MECHI NA TP MAZEMBE
1:26 AM |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment