CHELSEA WATANUA USIKU WA MANANE


NYOTA wa chelsea ambao wiki hii walifanya maajabu kwa kutinga robo fainali ya ligi ya mabigwa ulaya kwa kuitandika Napoli mabao 4-1 walisherekea ushindi mpaka usiku wa manane.  Ashley Cole na Didier Drogba walionekana wakiwa wameshika sigara aina ya cigar na waliuteka mji usiku wa jumatano. Mashujaa hao wa chelsea walituwa katika klabu usiku ya Aura huko Mayfair ili kusherekea ushindi wao.Klabu hiyo moja kati ya klabu za watu matajiri wa jijini london. Juan Mata, David Luiz, Michael Essien Florent Malouda, Bosingwa, Ivanovic nao walionekana wakifurahia maisha,lakina wakogwe John Terry na Lampard hawakuonekana mjini.baada ya kuondoka kwa kocha AVB wachezaji hao wameamua kuunganisha nguvu ili kuiokoa klabu yao. Wachezaji hao walikuwa na kila sababu ya kusherekea ushindi kwa kuwa wapenzi wa chelsea hawakuwa na uhakika wa kupiga hatua kubwa hasa baada ya kufugwa na Napoli mabao 3-1 huko Italy.Naye Terry alikaririwa akisema : Huu ni usiku mzuri kwetu inaonyesha ni kwa kiasi gani chelsea wapo makini.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment

Designed by Mustapha E.Hanya +255 732 575 718.