SIMBA WAMPA MILOVAN MIKANDA YA AL AHLI

KLABU ya Simba inatarajia kuinasa mikanda ya video ya mechi kati ya Al Ahli Shandi ya Sudan dhidi ya Ferroviário de Maputo kwa ajili ya kumkabidhi Kocha Milovan Circovic, kuitumia katika ufundishaji kabla ya kucheza na timu hiyo Aprili 29, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ezekiel Kamwaga ambaye ni Ofisa Habari wa Simba, amesema anatarajia kuipata mikanda hiyo ndani ya wiki hii.
 “Tunatarajia kuipata mikanda ya wapinzani wetu ndani ya wiki hii na tutamkabidhi kocha haraka ili aianzie kazi mapema, kama unavyojua Al Ahli ni timu ngumu, hivyo tutachukua ile mikanda ya mechi ya hivi karibuni ambapo walicheza wiki iliyopita dhidi ya Feraviario de Maputo,” alisema Kamwaga.
Al Ahli imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwatoa Ferroviário kwa jumla ya mabao 3-0. Simba imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora baada ya kuwatoa Waarabu wa ES Setif ya Algeria kwa faida ya bao la ugenini kufuatia mechi ya awali kushinda mabao 2-0 kabla ya kufungwa 3-1 ugenini.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment

Designed by Mustapha E.Hanya +255 732 575 718.