YANGA YAWAPA WACHEZAJI MILIONI 5 ZA VOCHA


KATIKA kuhakikisha inafanya vizuri katika mchezo wake wa ligi kesho dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Yanga kupitia kwa kamati yake ya utendaji, imewapa wachezaji wake shilingi milioni tano ili wafanye vizuri katika mchezo huo.
Yanga itaivaa Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani huku ikitaka kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya timu hiyo, kwani katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ilishinda kwa mabao 5-0.
Kwa mujibu wa kiongozi aliyehudhuria kikao cha kamati hiyo kilichofanyika kwa ghafla, jana mchana makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti Seif Ahmed, ilikutana na wachezaji wote wa timu hiyo na kuwapa mikakati na kiasi hicho cha fedha.
Kamati hiyo imewataka wachezaji wote kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo na ilisisitiza endapo watashinda, watapata zawadi nyingine ambayo hawakutaka kuiweka wazi katika kikao hicho.
“Unajua hakuna aliyekuwa anajua kama kamati hiyo itakutana leo na wachezaji, kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana na mara baada ya kuingia katika kikao hicho, kamati iliwataka wachezaji kufanya kweli katika mchezo huo na kupigana mpaka tupate ushindi,” kilisema chanzo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment

Designed by Mustapha E.Hanya +255 732 575 718.