WACHEZAJI wa klabu ya Simba, wamepewa shilingi milioni 25, kama mgao wa fedha za ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Wameupata hivi karibuni kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo ambao wametoa jumla ya shilingi milioni 40 kwa Simba.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kamati ya utendaji ya timu hiyo, Simba walipewa fedha hizo siku moja kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Azam.
Chanzo hicho kilisema fedha hizo tayari wamepatiwa na hivi sasa wanapanga jinsi ya kugawana kila mmoja, hasa wachezaji wote waliocheza ligi na kufanikisha ubingwa huo.
“Wachezaji wamepatiwa fedha zao shilingi milioni 25 za ubingwa katika zile milioni 40 tulizopewa na mdhamini wa ligi,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alikiri wachezaji hao kupewa fedha hizo ambazo ni sehemu ya ahadi kama wangechukua ubingwa.
“Ni kweli wachezaji wetu wamepatiwa fedha hizo, ambapo kila mchezaji aliyefanikisha ubingwa atapata ikiwa ni ahadi iliyotolewa na viongozi mwaka jana.
“Kiasi cha fedha walichopewa ni shilingi milioni 25 kati ya 40 za ubingwa tulizopata, nyingine zitaenda kwa uongozi, kiasi cha fedha watakachogawana ni siri hatuwezi kutangaza,” alisema Kamwaga
wachezaji simba wamwagiwa mamilioni
12:45 AM |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment