KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Khamis Kiiza, amesema ana zaidi ya aina 80 za kupiga mikwaju ya penalti.
Kiiza amekuwa akivutia mashabiki kila akipiga penalti, ambapo katika mchezo wa juzi dhidi ya Mafunzo, alipiga penalti ya tatu ambayo ilikuwa kivutio kuliko zote ikiwa na tofauti ndogo na ile aliyopiga kiungo wa Italia, Andrea Pirlo katika michuano ya Kombe la Euro 2012.
Akizungumza na Championi Jumatano muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kiiza maarufu kama Diego, alisema kikubwa kinachomfanya apige vizuri mikwaju hiyo ni kujiamini.
Alisema anajua vizuri jinsi ya kumdanganya kipa yeyote na kuwaonya makipa wengine wasikariri aina hiyo moja, kwani ni rahisi kwake kubadili muda wowote akitaka kufanya hivyo.
“Kwanza najiamini sana, huwa sina woga hata kidogo katika kupiga penalti, lakini kikubwa nina aina kama 80 hivi, sina tatizo katika hilo,” alisema Kiiza, raia wa Uganda na kuongeza:
“Zinapofika penalti na nikachaguliwa katika wale wanaotakiwa kupiga, huwa nasubiri tu zamu yangu ifike, lakini na makipa hawatakiwi kukariri aina yangu hii ya upigaji kwa sababu naweza kubadili wakati wowote, itategemea na kipa aliyepo langoni.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment