KAZI IPO TOTO NA YANGA CCM KIRUMBA MWANZA

YANGA imesema inajiandaa kuvuna pointi tatu kwa Toto African katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara utakaochezwa Aprili 15, mwaka huu, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Akizungumza na Championi Jumatano, katibu mkuu wa klabu hiyo, Selestine Mwesigwa, alisema mpaka sasa maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba ligi kwa sasa imekuwa ngumu hivyo ni lazima wakaze buti ili wapate pointi tatu na kurejesha matumaini ya ubingwa.
“Kama unavyojua ligi ipo ukingoni na katika msimamo hatujapishana sana kipointi, hivyo najua mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa sisi tunataka ubingwa na wao wanataka kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, itakuwa kama mbio za marathon.
“Hata hivyo, kikosi kipo vizuri kwa ajili ya mchezo huo na tumejipanga kuhakikisha tunachukua pointi zote,” alisema Mwesigwa.

Yanga ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 baada ya kushuka dimbani mara 21, wakati Toto ipo katika nafasi ya 11 baada ya kucheza michezo 21. Katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizo uliochezwa kwenye Dimba la Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilishinda kwa mabao 4-2.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment

Designed by Mustapha E.Hanya +255 732 575 718.