MTOTO JEREMY AKIENDESHA BASI BAADA YA DEREVA KUZIMIA

JEREMY WUITSCHICK, kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 13 kutoka Jimbo la Washington, Marekani, amepongezwa kwa kuweza kushika usukani wa basi la shule na kuliongoza baada ya dreva wake kuzimia Jumatatu wiki hii.
Kijana huyo alionekana kwenye video za kunasa matukio (CCTV) akiliendesha basi hilo hadi sehemu salama na kisha kuzima injini  yake baada ya kuanza kwenda mrama katika viunga vya mji wa Tacoma.
Wakati akilisimamisha basi hilo, ofisa mmoja wa shule ambaye alikuwa anashuhudia tukio hilo, alifika na kutoa huduma ya kumrudishia fahamu dreva huyo.  Vilevile, polisi walifika hapo na kuwaondoa wanafunzi 12 waliokuwa katika basi hilo.
“Kila mtu alikuwa ananiuliza nilifanyaje,” alisema…

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment

Designed by Mustapha E.Hanya +255 732 575 718.